Na Suzan Kanenka Mpanda
“Tuwalinde, tuwapende,
tuwaheshimu na kuwaenzi Mapdre”
Hayo
yamesemwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya Mhashamu Baba Askofu Gervas
Nyaisonga wakati wa Maadhimisho ya Misa takataifu ya kutoa daraja Takakatifu la
Upadre kwa Shemas John Muhuli na Filbert Baligwa misa ziliyofanyika katika
Parokia ya Karema na Buhingu.
Askofu
Mkuu katika mahubiri yake ameanza kwa kuwatafakarisha waumini na Mapdre juu ya
madaraka ya Padre ambapo ameeleza kuwa:-
Padre
katika baadhi ya maeneo anaogopwa na hii inatokana namna anavoishi na waumini
wake, wakati mwingine anaonekana na mwenye kunyang’anya haki za waumini, wakati
mwingine Padre hakubariki na waumini wake, na wakati mwingine Padre
anatafsiriwa kama mfadhili, mtoa misaada. Haya yote yatatokana na namna ambavyo
anaishi na kuwahudumia waumini wake.
Ameongeza
kuwa Padre sio jina bali ni hakikisho kwamba Yesu Kristo anaendelea kutenda
kazi zake ndani ya kanisa hivyo unapewa nguvu za kuweza kutenda kwa Jinan na
Nafsi ya Kristo, kupewa daraja takatifu la Upadre inamaana kwamba unapewa nguvu
za Kikristo, kama Mitume walivyopewa kibali cha kuwaondolea dhambi.
Amekumbusha
pia kuwa Padre ni chombo cha uumbaji mpya “ Ujio wa Yesu na sadaka vilitupa
ukombozi na tunapowabatiza waumini huo ni uumbaji mpya, nasi mapadre
tunayomamlaka ya kubatiza na kuwapatia watu uzima mpya. ( kwake yeye Napata
uzima mpya tena uzima wa milele).
“Shemas
John Muhuli na Filbert Baligwa mmepata daraja takatifu la Upadre na mnafanyika
kuwa chombo cha huduma, pelekeni amani kwa watu, nendeni mkawahudumie watu kwa
Roho na mamlaka mliyopewa na Kristo, Hudumieni wagonjwa, muwe mshauri, mle na kuongea na watu kwa upendo watendeeni waamini
sawa na matendo Ya Kristo, muwe mvumilivu, msiwe na hasira, wenye Hekima na
mpende watu, kwa kuishi hivyo mtafurahia utume siku zote.
Matarajio
ya kanisa kutokana na utume ni kuwa sadaka isiyo na mawaa, majitolea na
utumishi uliotukuka, ikiwa ni pamoja na kuipenda jumuiya ya Mapadre, Watawa na
waumini walei. mkienda kinyume na haya uhai wa Utume utazimika kama mshumaa…
Nanyi
waamini ambao mwenyezi Mungu anawatuma watumishi wake shambani watendeeni kama
mnavyowatendea watoto wenu na kuishi pamoja nao kwa upendo,wapeni ushirikiano,
muwampokee kwa moyo wenu wote, kubalini huduma a kikristo zitakazotolewa ili wawe
chombo bora cha Uumbaji Mpya.
Mwisho:
nawaombea heri na Baraka katika Upadre, acheni watu waone matendo yenu na sio
maneno.