Friday, February 22, 2019

UTAMBULISHO WA BLOG YA JIMBO



Muonekano wa Kanisa Kuu Mpanda


Jimbo katoliki la Mpanda

Tumsifu yesu kristo ……………………………………………………………………………………..

Napenda kuchukua fursa hii kuwaataarifu waumini wote juu  ya uanzishwaji wa blog ya jimbo ambayo iko tayari ( jimbokatolikimpanda.blogspot.com).
Blog hii ni matokeo ya maazimio ya wajumbe kutoka parokia 16 za Jimbo la Mpanda katika semina ya Mawasiliano na Mahusiano iliyofanyika Jimboni mpanda tarehe 8/01/2019 iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Habari Jimbo Suzan Kanenka na mdau wa Mawasiliano James Kapele na kuongozwa na Mhashamu Baba Askofu Gervas j Nyaisonga, Askofu wa Jimbo la Mpanda na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

Malengo mahususi .
·       
       Kupashana habari mbalimbali za Jimbo, Mafundisho ya dini hasa Kanisa Katoliki, Matukio, Sherehe, Sala, matangazo mbalimbali ya kanisa na kufahamu historia ya Jimbo kuanzia chimbuko lake.

·        Kutangaza neno la Mungu kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Kitengo cha habari na mawasiliano kinapenda kuwakaribisha wadau wote kuweza kuitembelea Blog hii ya Jimbo, kutoa mchango wa mawazo na ushauri baada ya kusoma habari na makala zitakazokuwa zikirushwa.
(blog ya Jimbo : jimbokatolikimpanda.blogspots.com)
TUMSIFU YESU KRISTO………. MILELE AMINA

3 comments:

  1. Hongereni sana wana jimbo la Mpanda kwa hatua hiyo. Mola awatangulie katika kufanikisha malngo hayo mahususi.

    ReplyDelete