Tuesday, July 16, 2019

UPADIRISHO WA SHEMAS FILBERT BALIGWA NA JOHN MUHULI



Na Suzan Kanenka Mpanda


“Tuwalinde, tuwapende, tuwaheshimu na kuwaenzi Mapdre”

Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga wakati wa Maadhimisho ya Misa takataifu ya kutoa daraja Takakatifu la Upadre kwa Shemas John Muhuli na Filbert Baligwa misa ziliyofanyika katika Parokia ya Karema na Buhingu.

Askofu Mkuu katika mahubiri yake ameanza kwa kuwatafakarisha waumini na Mapdre juu ya madaraka ya Padre ambapo ameeleza kuwa:-

Padre katika baadhi ya maeneo anaogopwa na hii inatokana namna anavoishi na waumini wake, wakati mwingine anaonekana na mwenye kunyang’anya haki za waumini, wakati mwingine Padre hakubariki na waumini wake, na wakati mwingine Padre anatafsiriwa kama mfadhili, mtoa misaada. Haya yote yatatokana na namna ambavyo anaishi na kuwahudumia waumini wake.

Ameongeza kuwa Padre sio jina bali ni hakikisho kwamba Yesu Kristo anaendelea kutenda kazi zake ndani ya kanisa hivyo unapewa nguvu za kuweza kutenda kwa Jinan na Nafsi ya Kristo, kupewa daraja takatifu la Upadre inamaana kwamba unapewa nguvu za Kikristo, kama Mitume walivyopewa kibali cha kuwaondolea dhambi.

Amekumbusha pia kuwa Padre ni chombo cha uumbaji mpya “ Ujio wa Yesu na sadaka vilitupa ukombozi na tunapowabatiza waumini huo ni uumbaji mpya, nasi mapadre tunayomamlaka ya kubatiza na kuwapatia watu uzima mpya. ( kwake yeye Napata uzima mpya tena uzima wa milele).

“Shemas John Muhuli na Filbert Baligwa mmepata daraja takatifu la Upadre na mnafanyika kuwa chombo cha huduma, pelekeni amani kwa watu, nendeni mkawahudumie watu kwa Roho na mamlaka mliyopewa na Kristo, Hudumieni wagonjwa, muwe mshauri, mle na  kuongea na watu kwa upendo watendeeni waamini sawa na matendo Ya Kristo, muwe mvumilivu, msiwe na hasira, wenye Hekima na mpende watu, kwa kuishi hivyo mtafurahia utume siku zote.

Matarajio ya kanisa kutokana na utume ni kuwa sadaka isiyo na mawaa, majitolea na utumishi uliotukuka, ikiwa ni pamoja na kuipenda jumuiya ya Mapadre, Watawa na waumini walei. mkienda kinyume na haya uhai wa Utume utazimika kama mshumaa…

Nanyi waamini ambao mwenyezi Mungu anawatuma watumishi wake shambani watendeeni kama mnavyowatendea watoto wenu na kuishi pamoja nao kwa upendo,wapeni ushirikiano, muwampokee kwa moyo wenu wote, kubalini huduma a kikristo zitakazotolewa ili wawe chombo bora cha Uumbaji Mpya.


Mwisho: nawaombea heri na Baraka katika Upadre, acheni watu waone matendo yenu na sio maneno.



No comments:

Post a Comment