Jimbo
katoliki la Mpanda
Tumsifu
yesu kristo ……………………………………………………………………………………..
Napenda
kuchukua fursa hii kuwaataarifu waumini wote juu ya uanzishwaji wa blog ya jimbo ambayo iko
tayari ( jimbokatolikimpanda.blogspot.com).
Blog hii ni matokeo ya maazimio ya wajumbe kutoka parokia 16 za Jimbo
la Mpanda katika semina ya Mawasiliano na Mahusiano iliyofanyika Jimboni mpanda
tarehe 8/01/2019 iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Habari Jimbo Suzan Kanenka na
mdau wa Mawasiliano James Kapele na kuongozwa na Mhashamu Baba Askofu Gervas j
Nyaisonga, Askofu wa Jimbo la Mpanda na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
Malengo mahususi .
·
Kupashana habari mbalimbali za Jimbo, Mafundisho ya dini hasa Kanisa Katoliki, Matukio, Sherehe, Sala, matangazo mbalimbali ya kanisa na kufahamu historia ya Jimbo kuanzia chimbuko lake.
Kupashana habari mbalimbali za Jimbo, Mafundisho ya dini hasa Kanisa Katoliki, Matukio, Sherehe, Sala, matangazo mbalimbali ya kanisa na kufahamu historia ya Jimbo kuanzia chimbuko lake.
·
Kutangaza neno la Mungu kwa njia
ya mitandao ya kijamii.
Kitengo
cha habari na mawasiliano kinapenda kuwakaribisha wadau wote kuweza kuitembelea
Blog hii ya Jimbo, kutoa mchango wa mawazo na ushauri baada ya kusoma habari na
makala zitakazokuwa zikirushwa.
(blog
ya Jimbo : jimbokatolikimpanda.blogspots.com)
TUMSIFU
YESU KRISTO………. MILELE AMINA